Mtandao wa eDaily kupitia ripota Brian Okoth umewataja wasanii watano kutoka Afrika wanaotajwa kuingiza pesa nyingi zaidi mwaka 2016.

Mikataba yake na makampuni makubwa kwenye kazi zake pia inazidi kumuweka sehemu nzuri kifedha.
Hakuna shaka kwamba Diamond ni mmoja kati ya wasanii wanaoingiza pesa nyingi kupitia muziki wao kwa sasa, na hili litaondoa utata kuhusu kiasi cha pesa alichotajwa kuwanacho staa huyu wa single ya Salome ambaye aliwahi kuzungumza na E!TV Jumapili ya, June 26 mwaka huu na ikaelezwa kuwa anamiliki pesa zinazozidi kiasi cha dola Milioni Nne za Marekani (Zaidi ya Bilioni 9 za Tanzania)
Pesa nyingi zinaelezwa kuingia kupitia shows alizofanya ndani ya Tanzania, East Africa na nje ya Afrika. Diamond Platnumz pia amekuwa balozi wa makampuni mengi makubwa ya biashara ikiwemo Vodacom, Cocacola, DSTV, Uber Taxi na Red Gold.
HII HAPA LIST KAMILI
1. P-Square (Tsh. Bilioni 277,752,822,639.34)
2. Akothee (Tsh. Bilioni 132,683,540,000.00)
3. Davido (Tsh. Bilioni 30,502,418,406.03)
4. Wizkid (Tsh. Bilioni 25,676,809,453.47)
5. Diamond Platnumz (Tsh. Bilioni 9,665,923,190.55)
0 comments:
Post a Comment